Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho Machi 21, 2018 atawaapisha Mabalozi wateule wawili aliowateua kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Rwanda na Urusi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli atamuapisha IGP-Mstaafu Ernest Jumbe Mangu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.
Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi Wateule hao itafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi.Post a Comment

 
Top