Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kuitaka jamii ya kitanzania na wengineo kuacha tabia ya kukata tamaa katika mambo wanayopanga kuyafanya kwani kitendo hicho kinaweza kupelekea kuumiza walioko nyuma yao bila ya wao kutegemea.

Jokate ametoa ushauri huo baada ya kuonekana dibwi kubwa la vijana wa leo kushindwa kufanya biashara au jambo lolote kwa kuhofia kuchekwa na marafiki wanaomzunguka na kupelekea kukata tamaa katika uthubutu wa kufanya maamuzi ambayo yangepelekea kuinua maisha yake kwa namna moja ama nyingine.

"Kabla hujakata tamaa hebu jiulize ni watu wangapi wanaokutegemea?, ni wangapi walioko nyuma yako ambao wanatiwa moyo na mafanikio yako, ni wangapi ambao wanaku-support?. Ndio ujue kuwa kukata kwako tamaa kutaumiza wengi hata kama unahisi kuchoka hebu jitie moyo kwa ajili ya hao", amesema Jokate.

Kwa upande mwingine, Jokate amesema mtu hapaswi kukata tamaa kwa jambo lolote madamu anapumua kwa madai bado anauwezo wa kufanikiwa katika kitu chake.


Post a Comment

 
Top