Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
index1
Waziri wa  Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliyeshika kipaza sauti akisikiliza kwa makini kero za migogoro ya ardhi kwa wakazi wa Dar es Salaa.

index2
Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar  es Salaam wakisubiri kutoa kero zao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  ambaye ameamua kuanzia Leo hadi keshokutwa kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekutana na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wanamigogoro mbalimbali ya ardhi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo.
 Hivyo wananchi wenye migogoro ya ardhi wamefika katika Wizara ya Ardhi jijini Dar es Salaam ambako ndiko inafanyika mikutano hiyo itakayochukua siku tatu mfurulizo . huku akiahidi kusikikiza migogoro yote kwa wale watakaofika kwake.
Wananchi mbalimbali wenye migogoro ya ardhi ikiwamo viwanja kuvamiwa, kuporwa,kuuzwa bila idhini na malalamiko ya hati kumilikiwa na zaidi ya mtu mmoja, Waziri Lukuvi ametumia nafasi hiyo kutatua mgogoro mmoja baada ya mwingine.
Jumla ya wakazi wa  Dar es  Salaam 250 wamejitokeza kutoa malalamiko yao ya migogoro ya ardhi na anaendelea kuisikiliza .
Mmoja ya walitoa malalamiko yao ya mgogoro wa ardhi ni Mohammed Salmin ambaye amesema kuna kiwanja ambacho anayo nyaraka zake lakini kuna mtu mwingine naye anasema ni kiwanja chake na amepewa hati kinyemela.
“Nimeenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kutoa malalamiko yangu lakini hakuna ambacho kinefanyika. Naomba Waziri unisaidie,”amesema.
Akijibu hilo Waziri Lukuvi amesema kiwanja hicho kina utata kwani Salmin ameambiwa kiwanja kipo eneo la barabara,
“Lakini maofisa ardhi wamempa mtu mwingine hati ya kiwanja hicho kinyemela na kuomba wasaidizi wake kulitafutia ufumbuzi,”amesema Waziri Lukuvi.
Mkazi wa jiji la Dar es salaam  Yusufu Azalia amemwambia anacho kiwanja na hati Kinondoni jijini Dar  es Salaam lakini ameshanga imejengwa nyumba ya kifahari na hajui nani amejenga.
Katika hilo Lukuvi amewaagiza maofisa wake kushughulikia kiwanja hicho ili mwenye hati halisi apewe kiwanja chake na nyumba iondolewe.
Wapo baadhi ya wakazi hao wameelezea namna nguvu ya feeha inavyotumika kudhulumu wenye hati halali za viwanja kiasi cha wengine kukamatwa na kufungwa bila sababu za msingi zaidi ya nguvu ya  fedha kupindisha ukweli.

Post a Comment

 
Top