Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
IMG_0009
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) katika ziara ya kushtukiza bandarini.
IMG_0030
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwa simu na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisini kwake.
IMG_0046
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiondoka katika eneo linalotolewa huduma za kibenki bandarini jana usiku mara baada ya kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.
IMG_0059
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifanya mahojiano na mmoja wa maofisa wa Bandari ya Dar es Salaam baada ya kukagua kama huduma zinatolewa saa 24 kama Serikali ilivyoelekeza.
IMG_9899
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Giliadi Ngewe.
IMG_9923
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), wakishuhudia moja ya wakala wa meli akiwa amefunga ofisi kinyume cha maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi saa 24.
……………….
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa jana usiku 
amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini mawakala 
wa meli wanaotoa huduma katika bandari hiyo hawafanyi kazi saa 24 kama Serikali 
ilivyoelekeza.
Prof. Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA) 
kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mawakala wote waliokiuka agizo la 
Serikali la kutoa huduma bandarini kwa saa 24.
“Kati ya Mawakala wa Meli nane ambao tumewatembelea usiku huu ni wakala mmoja 
tu ndiye tuliyemkuta akitoa huduma kwa saa 24 hivyo SUMATRA katika kipindi cha 
siku saba hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe kwa wote wanaokiuka 
utaratibu huu na nipewe ripoti ya hatua zilizochukuliwa,” alisema Waziri Prof. 
Mbarawa.
“Katika ukaguzi huu tumegunduwa kuwa mawakala wengi wanaacha watoa huduma 
wasiostahili, wakiwemo walinzi kufanya kazi nyakati za usiku ambao hawawezi 
kutoa huduma inayostahili usiku na kuendelea kutoa huduma asubuhi jambo ambalo 
sio sahihi,” amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na huduma zinazotolewa na taasisi za 
Serikali pamoja na benki, isipokuwa kwa taasisi ya Atomiki Enegy ambayo ameitaka 
ijieleze kwanini haifanyi kazi kwa saa 24 kama Serikali ilivyoagiza.
Profesa Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Maji Safi na Maji 
Taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) kuhakikisha maji safi na salama yanapatikana 
bandarini hapo kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoingia na kutoka na mapato 
yanayopatikana katika huduma hiyo ya maji kujulikana.
Waziri Mbarawa katika ziara yake ya kushtukiza aliambatana na maofisa wa 
SUMATRA ili kujionea wenyewe ukiukwaji wa agizo la Serikali na kusisitiza nia ya 
Serikali kuitaka Bandari ya Dar es Salaam kufanya kazi saa 24 ni kuiwezesha 
kushindana na bandari nyingine katika ukanda wa Bahari ya Hindi na kuongeza 
mapato.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Post a Comment

 
Top