Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
DSC_9999
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Ofisa wa Mradi wa Fumba Town Akif Ali Khamis, akitowa maelezo kwa Rais wakati akitembelea moja ya nyumba zilizojengwa katika eneo hilo wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi ikiwa ni sherehe za shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_9944
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Mji wa Kisasa Fumba Town, katika eneo la Nyamanzi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, hala hiyo imefanyika katika viwanja vya majengo hayo
DSC_9935
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa Fumba Town zilioko katika kijiji cha nyamanzi kutoka kwa Muwekezaji Sebastian Dietzold, kabla ya kuweka jiwe la msingi.
DSC_9900
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Fumba Town Sebastian Diatzod akitowa maelezi wakati alipotembelea kiwanda cha kutengenezea vifaa vya ujenzi wa nyumba hizo
DSC_9807
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakiangalia jinsi ya uunganishaji wa mbao wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi huo uliopo katika Kijiji cha Nyaminzi Zanzibar
DSC_9765
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea kiwanda cha utengenezaji wa malighafi ya ujenzi wa Nyumba za Kisasa Fumba Town, akipata maelezo kutoka kwa Muwekezaji wa Mradi huo. Sebastian Dietzold
DSC_0168
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Uwekezaji wa Mradi wa Mji wa Kisasa Fumba katika kijiji cha nyamanzi Wilaya ya Magharibi A Unguja, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 54.
DSC_0145
BAADHI ya Wageni waalikwa katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Mji wa Kisasa huko Fumba Town, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia wakati wa hafla hiyo ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DSC_0071
.WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rais Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kuzungumza katika hadhara hiyo na Wananchi wa Zanzibar wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la mradi huo huko nyamanzi Unguja.
DSC_0043
VIONGOZI wa jukwaa kuu wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa Fumba Town huko nyamanzi Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Picha na Ikulu

Post a Comment

 
Top