Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Tunda Man.
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva zao la Tip Top Connection, Tunda Man anadaiwa kutapeli mamilioni ya urithi ya msanii chipukizi, Asala Kipengele ‘Asala’.


Akizungumza na Full Shangwe, Asala alidai alitapeliwa fedha za urithi Milioni 30 alizompa Tunda Man ili amsaidie kimuziki lakini hadi sasa wamerekodi wimbo mmoja wa Subiri.

“Sitaki kumsikia Tunda kwa kile alichonifanyia, kanipiga sana hela za urithi kwa kujifanya meneja wangu lakini kumbe alikuwa amepanga kunitapeli,”alidai Asala na kuongeza;

“Kuna pesa kama milioni 30 ambayo nilimpatia kwa ajili ya muziki wangu lakini mpaka sasa sielewi chochote hata nikimpigia simu nyingi ni subiri, subiri.”
Full Shangwe lilimtafuta Tunda kujibu madai hayo alidai kwamba si kweli kwamba ametapeli hizo milioni 30.

Post a Comment

 
Top