Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Mamlaka ya Mapato nchini TRA, leo imefanya mnada wa magari ambayo wamiliki wake wameshindwa kuyalipia ushuru na ambayo yameegeshwa katika bandari ya Dar es Salaam.

Mnada huo umefanyika kama hatua ya kuhakikisha serikali inakusanya mapato kutoka kwa waagizaji wa magari hayo ambayo baadhi yake yamekaa bandarini hapo kwa muda mrefu zaidi ya ule unaokubalika kisheria.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Edward Kichere amesema katika mnada wa leo takribani magari 134 yamenadiwa na baadhi yake kununuliwa huku akiridhishwa na idadi ya umati wa watu waliojitokeza kununua magari hayo.
 

Post a Comment

 
Top