Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Thea  Afunguka Kuhusu Kufunga Ndoa Mwaka Huu 
STAA wa Filamu za Kibongo, Salome Urassa ‘Thea’ ameweka wazi kuwa, baada ya kutengana na mumewe Mike Sangu na kukaa kimya muda mrefu, sasa anatangaza rasmi kwamba mwaka huu ndio mwaka wake wa kuingia kwenye ndoa nyingine iwapo Mungu atamjalia.

Thea alisema kuwa, anavyoona yeye kwa mipango ya Mungu mwaka huu atapata ndoa nyingine kwani ni mwaka wa baraka kwake.

“Nitaolewa mwaka huu ni mwaka wa baraka na ninaamini Mungu atanijaalia kama ninavyomuomba, ili mambo na mipango niliyoipanga isiende tofauti,” alisema Thea.
 

Post a Comment

 
Top