Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jacqueline Wolper
HAKUNA mpenzi wa filamu za Kibongo am­baye hamjui Jacqueline Wolper, hii ni kwa saba­bu ya kujituma kwake kwenye kazi, hasa kuanzia kipindi kile tasnia ya Bongo Movie ilipokuwa juu, enzi za akina marehemu Kanumba mpaka leo.


Binafsi si shabiki sana wa filamu za Kibongo lakini mara chache ninazotazama kazi za hapa nyumbani, huwa navutiwa na uwezo wa huyu binti. Ukimta­zama kwa makini, utagundua kwamba Wolper anacho kipaji kikubwa cha uigizaji na ndani ya moyo wake anayo matamanio ya kufika mbali.


Ndiyo maana utamuona kuan­zia kwenye filamu za wakongwe, filamu za wasanii wachanga mpaka kwenye video za muziki za wasanii wa muziki wa kizazi kipya. Kwa hilo sina tatizo naye.

Upande wa pili wa maisha yake ya kimapenzi ndiko kwenye tatizo, Wolper hana historia ya kuvutia na matendo yake ya kuwaanika hovyo mitandaoni watu anaovunja nao amri ya sita kabla ya kuingia kwenye ndoa, huwa yanawafanya wengi wasi­yaone mafanikio yake kisanaa zaidi ya ‘skendo’ za kila kukicha
Wolper akiwa na Aliyekuwa mpenzi wake raia wa Kongo, Mwami Rajabu.
Maisha ya kimapenzi ni faragha na kila mtu anayo haki ya msingi kabisa ya faragha, hilo linafahamika lakini inapotokea mhusika mwenyewe kutojua maana ya faragha na kumwaga mambo yake ya ndani hadha­rani, tena kwa viapo na nadhiri, hapo ndipo penye tatizo.

Inafahamika wazi kwamba kwa mila za Kitanzania, tu­nategemea binti akishafikia umri wa kuolewa, muoaji atafuata hatua zinazotakiwa, ikiwa ni pamoja na kujitambulisha uk­weni, kutoa posa na kuchumbia kisha baadaye ndoa inafuata.
Hakuna anayetegemea kuona mwanamke wa Kitanzania, akiwa anabadilibadili wanaume huku akileta maigizo hata katika suala nyeti kama ndoa! Kuvalis­hana pete za uchumba si jambo la kufanyia mzaha kwa sababu hapo safari ya kuelekea kwenye unganiko takatifu kwa maana ya ndoa huwa umeanza.
Hivi karibuni kulizuka taarifa kwenye mitandao ya kijamii, zikimhusisha mwanadada huyu, Wolper kwamba anaenda ku­chumbiwa nyumbani kwa wazazi wake, Moshi mkoani Kiliman­jaro na Kibaha mkoani Pwani na mwanaume ambaye mpaka sasa bado hajulikan.
Wolper akiwa na Aliyekuwa mpenzi wake Brown.
Ukifuatilia kwa makini sarakasi za kimapenzi za Wolper, wakati akitoa taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii, zilikuwa ni siku chache tu tangu amwagane na aliyekuwa mpenzi wake, Brown.
Ukijiongeza kidogo, utagundua kwamba kitendo cha Wolper kutangaza kwamba anaenda kuchumbiwa, kinatoa tafsiri zaidi ya moja.

Kiuhalisia haiwezekani kwa muda mfupi tu ambao Wolper na Brown wamemwagana, tayari mwanadada huyo awe ameku­tana na mwanaume ambaye kwe­li yupo ‘serious’ anataka kwenda kumchumbia na kujitambulisha ukweni! HAIWEZEKANI.

Kwa wadadisi wa mambo, ni rahisi kugundua kwamba, aidha Wolper alifanya hivyo kwa saba­bu ya kumrusha roho mpenzi wake waliyeachana naye, Brown, au alifanya hivyo kwa lengo la kutaka umaarufu, wenyewe wanaita ‘kiki’.

Pia inawezekana kama ni kweli huyo mwanaume yupo na ameenda kumchumbia kama mwenyewe anavyodai, basi alikuwa akitoka na Brown kimapenzi lakini wakati huohuo akawa na mwanaume mwingine.
Kwa jinsi ninavyowajua wasanii wa Bongo Movie, kati ya hayo mambo matatu, moja linaweza kuwa kweli kwa Wolper na uwezekano mkubwa ni kwamba hakuna ndoa wala mchumba, bali ni KIKI!

Anataka azungumziwe, awe kwenye midomo ya watu, mitandao ya kijamii itawaliwe na stori zake, umaarufu wake uendelee kupaa! Unaweza kuona aina ya wasanii tulionao kwenye tasnia ya filamu Bongo. Yaani yupo tayari kujidhalilisha, tena hata kuwahusisha mpaka wa­zazi wake wakati anajua kabisa kwamba anachokizungumza ni uongo.

Nizungumze na wewe Wolper! Kama ulichokisema ni kweli, nakutakia kila la heri katika sa­fari yako ya ndoa unayoelekea kuianza, lakini kama ni kiki kama mlivyozoea kucheza na akili za watu, basi utakuwa umejishushia sana heshima yako, kimsingi huo ni ushamba.
Historia yako katika mapenzi inakuhukumu, kuanzia kipindi ul­ipokuwa na Abdallah Mtoro ‘Dal­las’, Putin, Mkongo, Harmonize, Brown na wengine ambao hatu­wajui (kama wapo), hata kama wao ndiyo wanakutenda ni rahisi watu kukutafsiri kwamba wewe si wife material! Hebu jaribu kuwa msiri kwa mambo yako ya ndani, acha watu waone vitendo tu.

Post a Comment

 
Top