Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Anastazia Mayunga ambaye ni Mama wa Peter Kibatala.
SIMANZI na majonzi vimetawala wakati wa misa ya kumuombea marehemu Anastazia Mayunga ambaye ni Mama wa Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa CHADEMA, Wakili Peter Kibatala,katika Parokia ya SUA, Mjini Morogoro leo Januari 13, 2017.


Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika (Mb) akitoa salamu za mwisho.
Viongozi mbalimbali wa Chadema, ndugu jamaa na marafiki wameungana na Kibatala katika kumuaga mama yake aliyefariki dunia juzi Alhamisi, Januari 11.
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick Ole Sosopi akitoa heshima za mwisho.
Baadhi ya viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika (Mb), Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrick Ole Sosopi, Godbless Lema, Susan Kiwanga, Meya Isaya Mwita na wengine.
Mhe. Susan Kiwanga (Mb) akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu.
Aidha, chama hicho kimeahirisha mkutano wake wa Kamati Kuu ya Chama uliokuwa ufanyike leo jijini Dar es Salaam ili kupisha shughuli ya kuaga mwili wa Mama Kibatala, hivyo mkutano huo utafanyika siku nyingine.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakitoa heshima za mwisho kwa Marehemu.

Viongozi wa Chadema wakishiriki ibada hiyo.

Post a Comment

 
Top