Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Huu ni Mwaka wa Mtoto Kwenye Ndoa Yangu na Tushaanza Kumtafuta- Shamsa Ford 
HUKU ndoa yake na mfanyabiashara Rashidi Said ‘Chid Mapenzi’ ikiwa na mwaka mmoja na miezi minne bila kupata mtoto, staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kufunguka kuwa mwaka huu wa 2018 ndiyo wa kupata mtoto.


Akichonga na Za Motomoto News, Shamsa alisema kama alivyowaahidi mashabiki wake tangu mwaka uliopita kwamba mwaka huu ndiyo atapata mtoto hivyo yupo kwenye harakati za kumtafuta na anaamini kwa uwezo wa Mungu atampata.

“Huu ndiyo mwaka wa mtoto na tayari mimi na mume wangu tumeshaanza kumtafuta, kikubwa tunamuomba Mungu atupatie kwani kwa akili na nguvu za kibinadamu hatuwezi na mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alisema Shamsa. 

 

Post a Comment

 
Top