Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Hivi karibuni umeibuka mzozo mkubwa kati ya mama mazazi wa mlimbwende Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga na mama mzazi wa msanii Diamond Platinumz, Mama Sandra, kufuatia kitendo cha mama Sandra kudaiwa kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kijana mdogo ambaye angeweza kuwa mtoto wake.


Kufuatia kitendo hicho, mama Hamisa amemjia juu mama Diamond akimsema kuwa anakubali kuolewa na kijana mdogo kama mwanaye, jambo ambalo siyo zuri kwa maadili ya kitanzania.

Shufaa aliongeza kuwa kuolewa na kijana mdogo aliyemuita kwa jina ‘serengeti boy’ ni kujivunjia heshima kitu ambacho hawezi kukifanya, ikiwa ni kwa faida ya wajukuu wake.

“Jamani mimi kama ni kuolewa basi nitaolewa na mtu mzima mwenzangu kwa sababu Serengeti Boy kwangu haiwezekani, nahitaji kuolewa kweli ila nitaolewa na mzee mwenzangu ili wajukuu wapate babu,” alieleza Shufaa lipohojiwa.

Mama mzazi wa Diamond, amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na kijana ambaye kwa umri ni sawa na mtoto wake anayeitwa Rally Jones jambo ambalo limeibua sintofahamu na kuamshan hisia za watu wengi, huku kila mmoja akiwa na maoni yake juu ya jambo hilo.

Post a Comment

 
Top