Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Image result for RUGEMARILA
Mfanyabiashara, James Rugemalila akiwa mahakamani.
MFANYABIASHARA, James Rugemalila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja.


Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo kuwa haujakamilika.

Baada ya kuelezwa hayo, mawakili wa utetezi, Michael Ngalo ameomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi wa kesi hiyo ama kama hawawezi waiondoe mahakamani.

Baada ya kuelezwa hayo, Rugemarila alinyoosha mkono ambapo alidai yeye ni mgonjwa wa kansa kwa miaka tisa sasa na amekuwa akipatiwa matibabu nchini India, lakini kwa sasa ugonjwa huo umejitokeza kwa njia ya uvimbe Katika sehemu za Siri.

Akiiambia mahakama kuhusu suala la wezi, Rugemarila alidai alishawasilisha nyaraka za ushahidi kwa Takukuru kwamba mwizi aliyeisababishia serikali hasara ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao waliisababishia serikali hasara ya Trillion 37.

Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16.

Naye mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi aliiambia mahakama ya Kisutu kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana, pia yupo tayari kutoa ushirikiano wowote ikiwemo nyaraka ili kubaini ukweli ni upi.

Baada ya kueleza hayo, wakili Swai alidai kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.

Akitoa ufafanuzi Hakimu Simba alisema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia ameutaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19,mwaka huu.

Post a Comment

 
Top