Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa kizazi kipya ambaye kwa sasa amerudi na ngoma aliyoipa jina 'Are U Ready' amejibu swali la wapenzi wengi wa burudani kwamba aliamua kuwa kimya kwa muda mrefu ili kumpatia nafasi msanii mwenzake Nandy na siyo kwamba alikuwa akimuogopa.

Ruby amesema kwamba ujio wa Nandy haukumpa Stress kwani anaamini msanii huyo ni mzuri na alikuwa akihitaji kusikika ndiyo maana hakutaka kukurupuka ili aanze kushindanishwa..
Aidha Ruby ameongeza kwamba anaamini kuwa Nandy anafanya aina muziki aliokuwa akifanya (Zouk) ndiyo maana hata watu wanadiriki kusema kwamba alikuja kuziba nafasi yake katika muziki na kuongeza kwamba tofauti yao ipo kwenye 'TONE' na 'SKALES' ndiyo maana aliamua kutulia ili kutafuta njia nyingine ili wasishindanishwe.
Pamoja na hayo Ruby amedai kwamba hapendi kushindanishwa na mtu yeyote na kwamba yeye katika maisha yake amezoea kujishindanisha mwenyewe.
Mbali na hayo Ruby ameongeza kwamba katika ukimya wake jambo lilokuwa likimuumiza sana ni jinsi ambavyo mashabiki zake walikuwa wakilalamika kwamba wamemmiss hali iliyokuwa inamfanya awe mnyonge na kushindwa cha kufanya.
 

Post a Comment

 
Top