Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Rappa kutoka kampuni ya Weusi, Johmakin amefunguka kwamba kama yupo kijana anatamani kuingia kwenye muziki kwa kutazama mafanikio yake, basi aache muziki kwani atakuwa hakifanyi hicho kitu kutoka ndani ya moyo wake.

Johmakin amesema kwamba mtu anayemfatilia afatilie muziki wake na siyo kutaka kujua muziki umempatia nini ingawa amekiri kwamba muziki ni biashara ambayo inamlipa sana. 
"My personal life style iko personal, Maisha yangu binafsi watu hawatakiwi kujua. Mimi ninachofanya ni hii sura ionekane kwenye TV, Brand ya Johmakini isimame, kufanya muziki mzuri basi. Lakini hayo mengine wacha yasijulikane. Sidhani kama namnyima mtu haki yake ya msingi kwa kutokuonyesha maisha yangu binafsi. Lakini muziki unanilipa sana. " Johmakin.
Akizungumzia kuhusu kubadilika kwenye tungo zake, Johmakin amesema kwamba ameamua kufuata jinsi ambavyo soko la muziki linataka lakini pia wakitaka kujua yeye ni Rappa wa aina gani lazima warudi nyuma  kutazama alipotokea.
"Unajua kwa sasa muziki umebadilika sana kwa sasa hatufanyi tena muziki mgumu inabidi ufanye muziki kuendana na wakati uliopo ndio maana hata mimi nimebadilika sana kwenye tungo zangu 'so' nimefanya kuendana na upepo wa sasa ulivyo" Johmakin.
 

Post a Comment

 
Top