Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii Quick Rocka amekanusha tetesi zilizokuwa zikiendelea mitandaoni kuwa yupo kwenye uhusiano mzito wa kimapenzi na Muigizaji Alice Kella.Rocka amekanusha tetesi hizo  na kupinga kwamba tetesi ambazo zilianza kusambazwa na msanii Alice kwa kuweka picha mtandaoni na kuandika maneno "mume wangu nampenda sana" ambayo  yalitafsiriwa kuwa ni wapenzi.

Aidha Quick Rocka amesema kwamba  hakuna mahusiano yoyote ya kimapenzi kati yao bali picha ambazo zilisambaa ni sehemu ya kazi zao za filamu.

"Mimi na Alice hatuna mahusiano yoyote yale na zile picha ni series tu ambayo tunaifanya ndio tulikuwa tunafanya photoshoot na hakuna kingine chochote kinachoendelea kati yetu zaidi ya kazi na Alice ni kama mdogo wangu hivyo watu wasichukulie tofauti" Quick

Msanii Quick Rocka kwa sasa  ni moja kati ya wasanii wakongwe na bado wanaendelea kufanya muziki na anafanya vizuri  huku akiwa anasimamia kundi la muziki liitwalo OMG. 

Post a Comment

 
Top