Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Patcho Mwamba ‘Tajiri’.

PREZIDAA wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Patcho Mwamba ‘Tajiri’, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita aligeuka mbogo baada ya kugusiwa tetesi za kumuachia nafasi hiyo mwanamuziki kipenzi cha wengi, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ aliyetoka kwenye kifungo cha maisha kwa msamaha wa Rais Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ hivi karibuni.

Papii Kocha.
Kufuatia kuzagaa kwa tetesi hizo kutoka kwa mashabiki wa burudani, Ijumaa Wikienda lilizungumza na Patcho kwenye onesho la bendi hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza- Mori, Dar ambapo aliwaka kuwa, hakuna mpango kama huo kwenye bendi hiyo.

“Asikudanganye mtu, hapa mimi ndiye prezidaa,” alisema Patcho kwa ukali. Kabla ya kwenda jela kwa miaka 13, Papii Kocha aliitumikia vyema bendi hiyo.

Post a Comment

 
Top