Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MSANII wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan ameibuka na kueleza kuwa ndani ya mwaka huu mpya wa 2018 ni lazima aandike historia kwani amechoka kila mwaka kuona wengine wanasonga mbele naye kubaki palepale.


Akizungumza na Risasi Jumamosi, Tiko alisema amejipanga kikamilifu kufanya kazi kwa bidii na kwa ubunifu zaidi kwani kila mwaka mastaa wanabaki walewale jambo ambalo linamuumiza kwa kuwa amekuwa akijitahidi lakini bado kiwango kile anachotaka kufika hajafikia hivyo ndani ya mwaka huu lazima aweke historia.

“Kila mwaka nimechoka kuona watu ambao hata hawafanyi kazi ya maana kwenye sanaa wakivuma na kuwa mastaa wakubwa wakati tupo wasanii ambao tunafanya kazi sana lakini hatuonekani, mwaka huu lazima nijulikane kila kona ya dunia kwa kuwa nimejipanga kufanya kazi kwa bidii na kufanya kolabo za muziki na filamu na wasanii wa nje ya Tanzania,” alisema Tiko.

Post a Comment

 
Top