Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Baada ya kupata misukosuko katika uongozi wake wa mwanzo na hata kufikia hatua ya kufukuzwa kwenye usimamizi wa MJ Records, Msanii Nini amesema kwamba lolote linaweza kutokea kati yake na Rapa Nay wa Mitego ikiwa kufanya kazi chini ya Free Nation.

Nini ameweka wazi hayo ikiwa ni  masaa machache baada ya kuachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Nay wa Mitego 'Niwe Dawa' na kusema kwamba ingawa amefanya kazi kwa kushirikiana na msanii huyo bado hana uongozi unaomsimamia japokuwa walishawahi kuzungumza jambo la kuwa chini ya lebo hiyo.
Akizungumza na kufanya kazi na Nay wa Mitego ambaye awali alihusishwa kutoka naye kimapenzi hadi kufikia sababu ya kufukuzwa MJ records, Nini amesema kwamba hakuna mahusiano yoyote kati yao yanayoendelea isipokuwa ni kazi tu na wala hakutegemea kufanya kazi na msanii huyo.
"Ni kweli yaliyotokea yametokea. Ukweli sijawahi kuwa na mahusiano na huyu kaka na hata kufanya kazi chini ya Free Nation. Hata Idea haikuwepo lakini vibe za studio zimetukutanisha kwa pamoja na sijamuimbia yeye ila maudhui ya wimbo ndo yanaonyesha kama ni 'dedication' kwake ingawa hakuna ukweli" Nini amesema.
Mwishoni mwa mwezi Octoba 2017, mtayarishaji wa muziki kutoka 'record label ya MJ' Daxo Chali aliweka wazi kuvunja mkataba na msanii Nini baada ya kubaini kuwa ana uhusiano ya kimapenzi na Nay wa Mitego.
 

Post a Comment

 
Top