Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Image result for Sasha Kassim

MWANADADA mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Sasha Kassim ambaye alikuwa anatarajia kuolewa siku chache zijazo amesema kuwa, ishu hiyo haipo tena na mahari hairudishwi.

Sasha Kassim akiwa kwenye pozi.
Akizungumza na Star Mix, Sasha alisema mwanaume huyo aliyemtaja kwa jina moja la Boniphace amejikuta akishindwa kuendelea naye sababu ya wivu, amekuwa akimuonea wivu picha anazoposti mtandaoni na kumtaka asitumie mitandao ya kijamii, jambo ambalo hayupo tayari kukubaliana nalo.

“Suala la ndoa halipo tena, yeye alinipata mtandaoni cha ajabu ananikataza kutumia mitandao nimeona sitoweza kuminywa uhuru wa maisha yangu kwa kiasi hicho, hivyo uchumba umevunjika na mpango wa kurudisha mahari haupo kabisaaa,”alisema.

Post a Comment

 
Top