Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Suzan Michael ‘Pretty Kind’.
MSANII wa filamu za Kibongo ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amemtaka mwanaume huyo atulie na aache kutapatapa na wanawake wa mjini.

Akizungumza na Za Motomoto News, Pretty alisema Nuh anatakiwa aache kutapatapa na wanawake wa mjini na ajikite katika kufanya kazi na kuachana na kutegemea kuhongwa na wanawake
Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
“Niliachana na Nuh maana nilishindwa kuwa na mwanaume ambaye anataka nimlee wakati nami ndiyo natafuta maisha, namshauri atulie sasa afanye kazi atafika mbali sana kuliko kutegemea kuhongwa,” alisema Pretty.
Nuh alipotafutwa kuhusu ishu hiyo, simu yake iliita bila kupokelewa.

Post a Comment

 
Top