Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MWANA-DADA anayeki-mbiza kwenye tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna’ amefungukia madai kuwa, siku chache zilizopita alikwenda Marekani kudanga na kukana vikali juu ya ishu hiyo.


Akizungumza na Showbiz Xtra kuhusu minong’ono hiyo, Dayna alisema, amesikia wengi wakimjadili kwamba safari yake hiyo siyo ya kikazi bali kaenda kutumika na kusema kuwa, ukweli ni kwamba aliamua kwenda kujichimbia huko kwa ajili ya shughuli zake za muziki na si kitu kingine.

“Najua wapo watu wachache ambao wametuharibia sifa hasa wanamuziki ambao wakienda Marekani nchi nyingine watu wanaanza kuwafikiria kwamba wamekwenda kwa ajili ya biashara ya ngono, hilo siyo kweli na wengine hususan mimi nilienda Marekani kwa ajili ya muziki tu,” alisema Dayna.

Post a Comment

 
Top