Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Gift Stanford ‘Gigy Money’.
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amesema kuwa kitendo cha muuza nyago Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuonekana akiwa mjamzito kimempa furaha kubwa na kuona ni jambo la ‘sapraizi’ kwake.


Akizungumza na Mikito Nusunusu, Mo Music alisema kuwa alivyoona picha za Gigy zikimuonyesha ana kibendi aliona kama ‘sapraizi’ kwake kutokana na mwanadada huyo alivyokuwa machachari huku muda mwingi akijinadi kuthamini mkwanja kwenye mapenzi
Moshi Katemi ‘Mo Music’ .
“Hili swala la Gigy limenikosha mno, kwanza alikuwa anasema anapenda mwanaume tajiri lakini jamaa aliye naye maisha yake ya kawaida tu, pia nimpongeze mshkaji kwa kumtuliza hadi kuamua kuzaa, nawasihi wasanii waige mfano wake, waache kuchoropoa mimba,” alisema.

Post a Comment

 
Top