Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Edward Lowassa leo January 8, 2018 wamefika katika hospitali ya Taifa Muhimbili kumjulia hali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru anapatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na mbwa wake.

Akizungumza nao Mzee Kingunge amesema anaendelea vizuri na panapo majaliwa jumatano atatoka na kurudi nyumbani kwake ili apate nafasi ya kushiriki kwenye mazishi ya mkewe licha ya kuwa na majeraha aliyoyapata yanayomsababishia maumivu.
Wakati madaktari wananisafisha haya majeraha nikawauliza, kama mimi nasikia maumivu hivi, Lissu je ana maumivu kiasi gani?, “Kingunge Ngombale Mwiru
Hali ya mwanasiasa huyo mkongwe inazidi kuimarika na anatarajia kutoka hospitalini hapo hivi karibuni ili kushiriki mazishi ya mkewe aliyefariki siku chache zilizopita.

Post a Comment

 
Top