Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Pam D na Mesen Selekta.
MSANII wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amejikuta kwenye wakati mgumu wa kumfariji ndugu yake ambaye pia ni msanii mwenzake, Mesen Selekta kutokana na kufiwa na mama yake ambaye alimfia mikononi mwake.

Akistorisha na Mikito Nusunusu, Pam D alisema mara kwa mara Mesen amekuwa akiweweseka akimtaka amueleze maneno ya mwisho ya mama yake aitwaye Lucy aliyomwambia kabla ya kifo chake kilichotokea siku chake zilizopita, sababu yeye ndiye aliyesikia kauli yake ya mwisho.
“Nipo kwenye wakati mgumu sana, mama yake Mesen mimi ni shangazi yangu na tulikuwa tunapendana mno, sasa kitendo cha kufia mikononi mwangu kimemfanya Mesen kila akiniangalia ajikute analia na kunihoji mara kwa mara dakika za mwisho shangazi alinieleza nini, inauma sana,” alisema.

Post a Comment

 
Top