Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii huyu maarufu kwa jina la Aunty Lulu.
KILA kukicha maisha yanabadilika na kuwa magumu hivyo hata katika ulimwengu wa mastaa wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali kwa kile wanachodai ni kurahisisha maisha yao.


Sanaa kwa sasa ni ngumu iwe ni muziki au filamu ambapo mastaa wengi wa kike wamekuwa wakiitumia mitandao ya kijamii kwa kujipiga picha za vituko mbalimbali huku wengine wakiwa nusu utupu ili tu kuongeza wafuasi wengi kwenye mitandao pamoja na kupata fursa mbalimbali za kazi za shoo au nyinginezo.

Wapo ambao wamekuwa wakifanya hivyo ili wapate mabwana kwani wanajikuta wakiitumia miili yao kama biashara ambapo wapo wanaofanikiwa kupata wanaume wa maana wa kuwasaidia maisha lakini wengine huishia kutumiwa na kuachwa
Jacqueline Wolper
Katika makala haya leo tunakuletea orodha ya mastaa ambao ni pasua kichwa mitandaoni kutokana na vituko vyao ambapo lengo lao hasa halijulikani moja kwa moja ni nini licha ya wengine kudai ni kwa ajili ya kuongeza wafuasi wengi kwenye kurasa zao kwani wakishawapata ni rahisi kutangaza kazi zao.

FAIDHA OMARY
Kwa jina la kisanii anatambulika kama Sister Fay ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya. Mwanamama huyu kwa sasa anaongoza kwa vituko mitandaoni hasa Instagram kwani amekuwa akijirekodi akiwa amevaa taulo au akikata mauno ya aibu kitu ambacho kinawashangaza wengi kwani zamani hakuwa hivyo.
Mwanamama huyu amewahi kukiri kwamba kukata kwake mauno kihasara na kukaa nusu utupu mitandaoni kumempa faida kwani amekuwa akipata shoo na mialiko mbalimbali nje ya nchi
LULU SEMAGONGO
Msanii huyu maarufu kwa jina la Aunty Lulu haishiwi matukio kwani kwa hivi sasa amekuwa akijipiga picha umbo lake na kutupia mitandaoni kuonyesha makalio yake.
Aunty Lulu amekuwa akifanya hivyo huku akiandika maneno ya kujisifia alivyo huku wafuasi wake wakimpongeza na baadhi yao kumshangaa na kumpa maneno makali kwamba inakuwaje analinadi umbo lake mitandaoni na ana lengo gani.

JACQUELINE WOLPER
Mwanadada huyu anaongoza kwa kuwa gumzo mitandaoni hasa kwa skendo yake ya kubadili wanaume. Wolper kila anapokuwa kwenye uhusiano amekuwa akiwaanika wapenzi wake muda mwingine wakiwa pamoja chumbani lakini anadumu nao kwa muda mfupi na kuachana.

Kwa sasa Wolper baada ya kuachana na kibenteni chake, Brown siku chache tu alitangaza mitandaoni kwamba anaolewa na anaenda kutolewa mahari kwa bibi yake huko Moshi jambo ambalo baadhi ya watu walilipinga kwani mwanaume mwenyewe hajulikani ni nani na kwamba ni mapema sana kwani ni siku chache tu ametangaza kuachana na mpenzi wake Brown kabla ya kutangaza kwamba anaolewa hivi karibuni
Sasha Kasim.
SASHA KASIM
Sasha ambaye ni muuza sura kwenye video za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva amekuwa akitupia video na picha za nusu utupu huku akikata mauno ambapo kutokana na umbo lake yaani makalio makubwa imekuwa ni aibu kwa baadhi ya watu na kusema kwamba anatangaza biashara ya kuuza mwili huku wengine hasa wanaume wakware wakifurahia
                                Mwanamuziki huyu wa Bongo Fleva, Amber Lulu.
FAIZA ALLY
Msanii huyu wa filamu ni mama wa watoto wawili lakini katika mitandao ya kijamii amekuwa gumzo kutokana na jinsi anavyopenda kuvaa nusu utupu pia hivi karibuni alijikuta mikononi mwa polisi kutokana na kuposti picha akiwa anajifungua.

Faiza maisha yake amekuwa akiishi Kizungu zaidi kwani anapenda kuweka wazi kila kitu mitandaoni pia kingine amekuwa akimshambulia kila wakati baba wa mtoto wake ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ hali ambayo imemfanya Faiza kuwa gumzo sana kwenye mitandao kutokana na vituko vyake hivyo.

AMBER LULU
Mwanamuziki huyu wa Bongo Fleva amekuwa akichafua hali ya hewa katika mitandao ya kijamii kwa kuposti picha mbalimbali za nusu utupu bila kujali kwamba yeye ni kioo cha jamii au laa.

Kuna wakati alipiga picha akiwa nusu utupu na msanii mwenzake Young D na kuwashangaza watu kwani kwa utamaduni Tanzania hiyo haikubaliki.

JANE RIMOY
Huyu yeye ni modo, licha ya serikali kuzuia picha za utupu, yeye ameendelea kuziposti hata baada ya Rais Dk John Pombe Magufuli kuzitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua.
Mrembo huyu maarufu kwa jina la Sanchi, amekuwa akiweka picha zake za utupu na kuonesha umbo huku akiwa maarufu zaidi kutokana na kalio lake kubwa.

Post a Comment

 
Top