Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa muziki Bongo, Young Killer amesema amesikitishwa na kitendo cha kolabo yake na Khaligraph Jones kuvuja.

Rapper huyo ameiambia 5 Selekt kuwa ngoma hiyo ilikuwa kwenye mipango mikubwa ambayo si kwa wakati huu.
“Napenda kusikitika na kutoa taarifa hizi rasmi kutokana na wimbo ambao nimefanya Khaligraph Jones kuwa umevuja ni kitu ambacho mwenyewe kimenishangaza hata Khaligraph mwenyewe kanicheki kiukweli kwa namna moja au nyingine imeni- disappoint,” amesema.
“Sijui imetoka kwa mazingira gani kwa style gani kwa sababu ni wimbo ulikuwa na mipango mikubwa, ilikuwa ni demo imekuja katika wakati ambao sio,” amesisitiza.
Ngoma ambayo Young Killer anadai imevuja inakwenda kwa jina la How we Do.


Post a Comment

 
Top