Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya waombolezaji wakimpa pole Kingunge Ngombale Mwiru, nyumbani kwake Mwananyamala muda mfupi kabla ya kuaga mwili wa marehemu Perasi Ngombale Mwiru na kuelekea kanisani, St. Peter, Oysterbay kwa ajili ya misa.
MWANASIASA mkongwe nchini, Mzee Kingunge Kombale Mwiru amemsindikiza mkewe Peras Ngombale Mwiru katika safari yake ya mwisho ambaye amezikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Januari 11, 2018 jioni

Mzee Kingunge akisikiliza maelezo ya mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya msiba (hayupo pichani)
Kingunge aliyekuwa amelazwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya taifa Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake, alitolewa hospitalini baada ya kupata nafuu ili kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki ili kushiriki mazishi ya mkewe aliyefariki dunia Januari 4, mwaka huu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa ugonjwa wa kupooza
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji (wa pili kulia) akifuatilia taratibu za msiba nyumbani kwa Kingunge.
Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba, Frederick Sumaye na Edward Lowassa pia wameungana na mamia ya ndugu, jamaa katika tukio la kuaga mwili wa mke wa Mzee Kingunge.
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Semamba Makinda akimpa pole mmoja wa wanafamilia ya wafiwa. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa.
Tukio la kuaga mwili huo leo Alhamisi limetanguliwa na matukio ya pole kwa familia ya mzee Kingunge.

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likiingizwa kanisani, Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay kwa ajili ya misa.
Baada ya tukio zima la kuaga hapo nyumbani, mwili huo utapelekwa katika kanisa la Mtakatifu Peter kwa ajili ya ibada Maalumu kabla ya kuelekea Makaburi ya Kinondoni.

Jeneza lenye mwili wa marehemu, muda mfupi kabla ya kuanza misa.

Mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akifuatilia misa kanisani.

Padri akiongoza misa kanisani hapo.

Spika Mstaafu, Anne Makinda ( wa tatu kulia) akisikiliza misa kanisani.

Mzee Kingunge akiwa pamoja na wanafamilia yake, muda mfupi kabla ya kuaga mwili wa marehemu mkewe nyumbani kwake.

Waombolezaji wakifuatilia taratiba za msiba nyumbani kwa marehemu.

Picha ndogo ya marehemu Perasi enzi za uhai wake.

Mama Maria Nyerere akiaga mwili wa marehemu kanisani.

Jaji Mkuu Mstaafu, Chande Othman akiaga mwili wa marehemu.

Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu likiondoka kanisani hapo kuelekea makaburini, Kinondoni kwa ajili ya mazishi.

Post a Comment

 
Top