Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
1
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel afanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro na kutembelea kiwanda cha 21 Century pamoja na kiwanda cha Abood Seed Oil Industry Ltd vyote vya mjini Morogoro.
katika hotuba yake Prof. Elisante amesifu utendaji wa kazi wa viwanda hivi na kluwataka kuongeza juhudi ya uzalishaji wenye tija na kuthamini wafanyakazi.
 
Katibu Mkuu ameeleza kuwa Serikali inapenda kuona muelekeo mzuri wa Viwanda kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 hivyo ni jukumu la wenye Viwanda kuongeza uzalishaji wenye tija ambapo kwa upande wa serikali kazi yetu ni kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuondoa vikwazo vya kufanya shughuli.
1
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akipokelewa na mtendaji mkuu wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
2
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
3
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akiangalia pamba iliyosokotwa kushoto kwake ni ndugu Gevaronge Miyombe, Mchumi Wizara ya Viwanda na kulia kwa katibu mkuu ni ndugu Deus Rwegasira Msimamizi Mkuu, Idara ya Usokotaji katika kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
4
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akiangalia mashine ya usokotaji wa nyuzi pembeni ni ndugu Deus Rwegasira, Msimamizi Mkuu -Idara ya Usokotaji katika kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
5
Wafanyakazi wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogor
6
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro.
7
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akizunguka katika kiwanda cha ABOOD SEED OIL INDUSTRY LTD akiangalia utendaji kazi wa kiwanda hicho mapema hii leo.
8
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel akimsikiliza mwekezaji wa kiwanda cha Abood Seed Oil Industry Ltd Mbunge jimbo la Morogoro Mjini ndugu Abdulaziz Mohamed Abood wakati wa majadiliano mara baada ya kutembelea kiwanda hicho.
9
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kiwanda cha Abood Seed Oil Industry Ltd. cha mjini Morogoro.
10
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel, akizungumza na wamiliki wa kiwanda cha 21 Century cha mjini Morogoro (Hawapo pichani) pembeni ni ndugu Ernest R. Mkongo – Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya uchumi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Post a Comment

 
Top