Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
1
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (kulia), akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ziara ya kikazi ili kuona namna Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) inavyofanyakazi zake pamoja kujadiliana namna yakuimarisha eneo la utoaji Haki Jinai pamoja na ubadilishanaji wa taarifa, anayefuatia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.

2
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, pamoja na Maofisa wa Jeshi hilo wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (katikati), akitoa neno wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo ili kuona namna Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) inavyofanyakazi zake pamoja kujadiliana namna yakuimarisha eneo la utoaji Haki Jinai pamoja na ubadilishanaji wa taarifa.
3
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome (kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (wa pili kulia) na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele  (kulia) wakiteta jambo wakati walipokuwa kwenye moja ya ofisi ya Uchunguzi wa Kisayansi (Forensic Bureau) Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jana, ili kuona namna Kamisheni hiyo inavyofanyakazi zake.
Picha na Jeshi la Polisi.

Post a Comment

 
Top