Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa muziki hip hop wa Bongo, JCB amekosoa mfumo ambao unadaiwa kuwepo katika Bongo Flava ambao ni wasanii kulipa fedha ili kupata interview na nyimbo zao kuchezwa katika vyombo vya habari hasa redio na runinga.

Rapper huyo kuwa kitu hicho si kizuri kwani licha ya kuua muziki inaweka uzibe kwa wasanii wachanga.
“Hiyo kitu ni zuluma, ni utapeli yaani vitu ambavyo havitakiwa kuwepo na ni kweli hiyo system ipo Tanzania muda huu, nasikia ukitaka interview utoe hela, ili wimbo wako uchezwe utoe hela,” amesema JCB.
JCB ameongeza kuwa kutokana na tabia hiyo kuanza kushamiri ndio sababu miaka ya hivi karibuni hakuna msanii underground aliyetoka na kufanya vizuri bali wanaosikika ni wale wale ambao tayari wanajuana na baadhi ya watu katika vyombo vya habari.

Post a Comment

 
Top