Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baada ya kuvuja kwa picha za Mtangazaji wa Clouds FM, Diva ikimuonesha akizozana na mpenzi wake Heri Muziki huku picha nyingine zikimuonesha akivuja damu, mrembo huyo amekiri wazi kuwa ni kweli ugomvi  huo ulitokea na picha ni zake.
Diva amesema tukio hilo lilitokea wiki iliyopita wakiwa maeneo ya Kinondoni na kudai kuwa wakati wakizozana walirekodiwa na mtu aliyekuwa karibu nao na ndiye aliyevujisha picha hizo.
Akieleza chanzo cha vurugu hizo na mpenzi wake amesema lilikuwa ni tukio la wivu ambapo Heri Muziki alikuwa anamtuhumu kumsaliti na baadae kufuta picha zote alizopiga na Diva kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Heri amefuta picha zinazonihusu mimi katika page yake ya Instagram anyway ni maamuzi yake najua hilo limetokea baada ya tukio lililotokea wiki iliyopita, He is grown up he knows nini anafanya. Mimi sijafuta hata picha moja zinazomuhusu yeye kwenye ukurasa wangu i always keep memories,“amesema Diva kwenye mahojiano yake na Bongo5 huku akifafanua skendo ya usaliti
Mimi sijawahi kumsaliti Heri sijawahi fanya hivyo hata mara moja, i’m very faithful in my life ninapokuwa kwenye mahusiano. He has his own issues going on in his life but that has nothing to do with me, siwezi kumzungumzia kwa mabaya namheshimu sana amekuwa na mimi kwenye kipindi cha shida na raha so haitakuja tokea mimi kukaa na kumzungumzia kwa mabaya, then maisha yangu ya mapenzi nataka yawe private.“amesema Diva.
Hata hivyo, Diva baada ya tukio ametoa msimamo wake juu ya mapenzi yake na Heri Muziki kwa sasa ambapo amesema kuwa kukoseana ni vitu vya kawaida.
In my life or relationship kukoseana kupo. Beyonce na Jay Z watu walihisi wale walikuwa perfect couple but dunia ilishuhudia, so that normal i keep the positive life coz mwisho wa siku Heri anaweza kuja kuwa mzazi mwenzangu. He is a good guy and i hope watu wataheshimu maisha ya watu hasa ya kimapenzi.“amesema Diva na kuwaomba radhi mashabiki wake na wafanyakazi wenzake wa Clouds FM.
Sorry for my disapointment waliyoipata mashabiki wangu, wafanyakazi wenzangu na ndugu jamaa na marafiki baada ya picha hizo kusambaa, sh*t happens and life goes on.“amemaliza Diva.

Post a Comment

 
Top