Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mwenyekiti Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Hashim Rungwe Spunda amefunguka na kusema hakuna tatizo Lowassa kukutana na Rais Magufuli lakini amedai kuwa ni lazima tujue watu hao walipokutana Ikulu walizungumza nini kwani sasa imebaki siri yao.

Rungwe amesema hayo alipohojiwa na moja ya chombo cha habari nchini na kudai kuwa Lowassa hapaswi kulaumiwa ila tu ni lazima aweke bayana kile ambacho alikaaa na kuzungumza na Mhe. Rais Magufuli ili Watanzania wajue jambo hilo lina maslahi wapi. 
"Hatujui walichozungumza maana mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye anafahamu watu hao wamezungumza nini, Rais Magufuli mwenyewe hakusema nini wamezungumza na Lowassa hata Lowassa mwenyewe hajasema mpaka sasa nini amezungumza na Rais Magufuli hivyo imebaki ni siri yao, sasa hii siri yao lazima tuitafute na kuijua baadaye kama ina faidi kwa upande wetu au ina faida upande ule moja kwa moja" alisema Rungwe 
Aidha Rungwe amesema kuwa kwa watu ambao wanaona bado Serikali ya awamu ya tano haijibu hoja na kutatua matatizo ya wananchi wanapaswa kuendelea kupiga kelele na wale ambao wanaona Mhe. Rais Magufuli ametekeleza mambo nao waendelee kumuunga mkono. 
"Wananchi wanaoendelea kulalamika tuendelee kulalamika na wale wanaona kisha maliza kila kitu waende wakamuunge mkono hicho alichokimaliza maana hakuna alichomaliza rushwa bado inalalamikiwa, hospitali dawa bado zinalalamikiwa, hatukatai nyinyi kumpamba lakini kuna misingi sisi tunataka vitu vionekane"

Post a Comment

 
Top