Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Breaking News: Bavicha Wafunguka Kuhusu Lowassa Kukutana na Rais Magufuli  Ikulu 
Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) limesema kauli za kumsifia Rais John Magufuli zilizotolewa na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 sio msimamo wa Chama hicho na wala hawaitambui.


Katibu Mkuu wa Bavicha, Mwita Julius alisema wao kama Baraza wanaungana na kauli ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alisema wao kama chama hawatambui kauli za Lowassa.

" Sisi kama chama tunashangaa katika wakati ambao Taifa halijui mustakabali wake wa kiuchumi, wabunge wa upinzani wanafukuzwa bungeni, wanasiasa wanashambuliwa kwa risasi Mjumbe wa kamati kuu unapataje ujasiri wa kuisifia Serikali?,

" Hatuna hofu yeyote maana zinasikika kuwa Lowassa anaweza kurudi CCM, hayo ni maneno tu na wala hatuna hofu yeyote sisi kama Chama tumewahi kupitia misukosuko mikubwa, na hata sasa tunaona namna ambavyo viongozi wetu wananunuliwa, sisi tupo imara sana na pia tuna uhakika hatoondoka," alisema Mwita.

Aliongeza kuwa suala la Lowassa kwenda Ikulu kuonana na Rais Magufuli wao hawana shida nayo ingawa wanashangazwa na kauli ambazo alizitoa baada ya kufanya mazungumzo hayo. 

Post a Comment

 
Top