Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa Bongo Muvi, Wastara Juma.
MENEJA na aliyekuwa mpenzi wa msanii wa Bongo Muvi, Wastara Juma, Bond Suleiman amefunguka kuwa mwaka 2017 ulikuwa ni mchungu sana kwake, baada ya kuhusishwa na tukio la ujambazi na ishu ya kuachana na Wastar

Wastara Juma akiwa na Bond Suleiman.
Akizungumza na Za Motomoto, Bond alisema kuwa kwenye uhusiano aliumia sana kumuacha Wastara hasa baada ya kumuona ni kama anataka mafanikio ya haraka wakati yeye uchumi ulikuwa umeyumba.

“Mimi ndiye niliyemuacha Wastara na kuamua kuondoka zangu na kwenda kufanya maisha yangu mengine kwa sababu niliona kama namkosesha amani na pia alitaka mafanikio ya haraka wakati uchumi wangu uliyumba. Pia ishu ya kuhusishwa kwenye ujambazi ilinitesa sana kwani nilikaa selo siku ishirini ila nashukuru polisi waliujua ukweli nikawa huru,”alisema Bond.

Post a Comment

 
Top