Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Ngereza amesema kwamba hawajampatia adhabu yoyote msanii Gigy Money kwa sababu siyo wao waliomwita na badala yake akaonane na Naibu Waziri wa sanaa habari na Utamaduni Mh. Juliana Shonza.

Akizungumza na mfupi baada ya msanii huyo kutoka BASATA, Mh. Ngereza amesema kwamba wao walichokuwa wakisisitiza kwa msanii huyo ni kuitikia wito wa Mh Shonza na siyo kumpatia hukumu.
Kwa upande wa Msanii Gigy Money amedai kwamba hakuna uhuru tena  na atajitahidi kwenda kuonana na Naibu Waziri kama jinsi ambavyo BASATA walivyopmtaka kufanya.
"There is No freedom....Hakuna uhuru tena....Hakuna. Nitaongea na Naibu Waziri kama wanavyodai. Mtu anakuja kukujaji picha ya 'March' last Year...wananiambia pia hata kipindi nikiwa video vixen nilikuwa natakiwa kujitambulisha Basata, sijawahi kusikia haki ya 'video vixeni' mara ngapi nimelia mitandaoni kwa kulipwa elfu 20. Nitaongea naye naamini haki yangu itapatikana". Gigy Money
Gigy Money ni moja ya wasanii ambao waliitwa jana na Naibu Waziri Juliana Shoonza kufika ofisini kwake kwa kukiuka maadili kwenye kazi zake za sanaa.
CHANZO NA EATV
 
 

Post a Comment

 
Top