Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa kizazi kipya katika mtindo wa mduara, Ally Tall ' AT' amewaomba radhi mashabiki na wadau wa burudani kwa kushindwa kuvunja tuzo yake kama jinsi alivyoahidi kwa madai kuwa hakujua kama tuzo hiyo ni mali ya Baraza la Sanaa nchini (BASATA).

AT amesema kwamba hataweza kuwavunjia BASATA heshima kwa kuvunja tuzo hizo na mwanzo alisema kwamba alitangaza kuzivunja kwa kudai kwamba hazina maana.
"Naomba kutengua kauli ya mahojiano niliofanya miezi6 iliopita ya kua nitavunja Tuzo hadharani hii ni baada ya kufuatilia kwa kina na kupata maelezo ya kujitosheleza yenye mashiko mazuri. Tuzo ni mali ya BASATA na sitawavunjia heshima ni waadilifu na wanatupenda wasanii wote" AT
Ameongeza kwamba "Utofauti uliopo ni sikujua kuwa waandaaji sio wamiliki wa hilo na mimi niwaombe radhi watanzania kama binaadamu nina mapungufu yangu mnisamehe kwa kila baya nililowakosea".Amesema AT
Miezi Sita iliyopita AT alitangaza kuvunja Tuzo aliyowahi kupokea hapa nyumba kwa madai kuwa haoni faida yake.
 

Post a Comment

 
Top