Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Mwanamuziki anayefanya vizuri na ngoma ya 'Sometimes', Baraka The Prince amesema kwamba kama angerudi nchini bila kwenda kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa Nairobi akijiuguza majeraha ya risasi, basi nafsi ingemsuta sana.
Akizungumza baada ya kurejea kutoka Nairobi ambako alikuwa ameenda kufanya 'show' ya mkesha wa mwaka mpya,  Baraka amesema kwamba alipoamua kwenda kumuona Lissu hospitali alimfikiria Lissu kama mtanzania na kiongozi anayetazamwa na wengi na kufafanua kwamba kwenda kwake kusihusishwe na siasa kwani yeye siyo mwanachama wa chama chochote.
Akizidi kufafanua Baraka amesema kwamba, mbali na kuwa Lissu ni kiongozi lakini kwa wakati huu anahitaji faraja kutoka kwa watanzania wote kwa ujumla kwani anavyofahamu yeye mgonjwa anaishi kwa saikolojia na anapotembelewa ndipo anapata matumaini ya kupona zaidi.
"Nimeenda kumuona Mh. Lissu kama mtanzania yoyote yule ambaye ningejua kwamba yupo hospitalini pale nisingeacha kwenda hata kama angekuwa shabiki. Nafsi ingenisuta sana kama ningeondoka bila kwenda kumuona, unajua hata yeye angekuja kusikia kwamba nimefika mpaka pale na sijaenda siku nyingine tungekutana mtaani ingekuwaje, japo hiyo haikuwa lengo langu. Mimi napenda kuishi kwa upendo" amesema Baraka.
Akizungumzia kuhusu walichoongea, Baraka amesema kwamba yeye pamoja na Mh. Lissu walizungumzia zaidi muziki wa msanii huyo na pia kumpa shukrani azilete kwa watanzania kwa maombi ambayo wanamuombea.
Baraka The Prince anakuwa  msanii wa pili kwenda kumuona Tundu Lissu akiwa hospitalini huko jijini Nairobi akiwa anatokea Turkana kwenye show mwanzoni mwa mwaka huu, msanii wa kwanza alikuwa Matonya.
Lissu alipelekwa jijini Nairobi usiku wa Septemba 7, 2017 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika viunga vya nyumbani kwake mjini Dodoma akiwa ametokea Bungeni.
 
 CHANZO NA BONGO 5

Post a Comment

 
Top