Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
BAADA ya msanii wa muziki, Rehema Chalamila ‘Ray C’ kumuandikia ujumbe Rais John Pombe Magufuli kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anaomba wanaoingia kwenye nyumba za wageni wawe wameolewa na waoneshe cheti cha ndoa mlangoni staa mwenzake, Lungi Maulanga ameibuka na kumshambulia vikali na kudai kuwa hakupaswa kuongea hivyo kwa sababu yeye hana ndoa

Lungi Maulanga.
Akiongea na Risasi Jumamosi Lungi alisema kuwa Ray C hakutakiwa kuongea hayo wakati yeye bado hajaolewa angeolewa kwanza ndiyo akaanza kuongea maneno hayo.

“Ninavyomjua Ray C bado hajaolewa, sasa hayo anayomwambia mheshimiwa alitakiwa kwanza kuyafanyia kazi yeye kwa sababu ninao uhakika kuwa hata yeye anaingia nyumba za wageni na wala hajaolewa, atupe mfano kwanza kwa sababu mimi najua sheria hatungi yeye,” alisema Lungi ambaye haikufahamika ni kwa nini alikerwa na jambo hilo kwa sababu yeye ni mama mwenye watoto wanne tena wote ni wa kike.

Post a Comment

 
Top