Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nyota huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 34 amesema kuwa anaipenda nchi yake na yuko tayari katika uteuzi kwaajili ya kuitumikia timu hiyo.

Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure ametangaza kurejea katika timu yake ya Taifa ya Ivory Coast ikiwa ni mwaka mmoja na miezi mitatu toka atangaze kustaafu kuichezea timu hiyo.
Toure ambaye amecheza mechi tatu tu za Ligi kuu ya England akiwa na klabu yake ya Manchester City amesema anataka kuwasaidia wachezaji chipukizi katika kikosi hicho cha timu ya Taifa ya Ivory Coast.
Uamzi huo wa Yaya umekuja ikiwa ni muda mchache tu umepita ikiwa nchi yake ya Ivory Coast imeshidwa kufuzu katika fainali za kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

Post a Comment

 
Top