Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Jafo Atoa Agizo Mkurugenzi wa Halmashauri Kuchunguzwa  
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini,  Sudi Mussa Mpiri atafanyiwa uchunguzi kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.


Agizo hilo la kufanyiwa uchunguzi limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa mkurugenzi huyo baada ya kutoridhishwa na miradi ya maendeleo aliyoitembelea.

Mussa Mpiri anadaiwa kushindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani. Imeelezwa pia zaidi ya asilimia 90 ya matumizi ya pesa hizo hayafahamiki hivyo kutia shaka juu ya utendaji wake.Kufuatia hatua hiyo Waziri Jafo, ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka ndani ya Halmashauri hiyo kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa Mkurugenzi huyo.

Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia  rasilimali za Halmashauri hiyo.

Post a Comment

 
Top