Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
HABARI ya mjini ni kwamba viongozi wa taasisi ya Uzalendo Kwanza wameamua kujiweka pembeni kwa kile walichodai kwamba hawamuelewi mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.


Chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa viongozi wote akiwemo aliyekuwa makamu mwenyekiti, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na wengine kama Halima Yahya ‘Davina’, Salom Urassa ‘Thea’, Sabrina Rupia ‘Cathy’ waliamua kujiweka pembeni kwa kile wanachodai kuwa Steve Nyerere anajinufaisha mwenyewe kwani anafanya mambo kibao bila kuwashirikisha.

Baada ya kupata habari hizo, Risasi Jumamosi liliwatafuta viongozi hao ambao walikiri kujiweka pembeni kwa sababu hawamwelewi Steve na kudai kuwa ili wasije kugombana wameamua kujiengua mapema wafanye mambo yao mengine ingawa haki zao zipo palepale kwani ndiyo waanzilishi. Kwa upande wa Steve alipoulizwa kuhusiana na hilo alijibu kwa ufupi ‘hakuna kitu kama hicho’.

Post a Comment

 
Top