Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ramadhan Kailima ambaye ameeleza kuwa mgombea ubunge wa CHADEMA kwenye jimbo la Singida Kaskazini wanayedai kuwa sio wa kwao kwa sababu hakupitishwa na Kamati kuu ya CHADEMA, alikidhi vigezo vyote vya kupitishwa na tume kuwa mgombea.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa Katiba, hakuna mgombea atakayeteuliwa kwa nafasi yoyote ya ubunge isipokuwa amedhaminiwa na chama cha siasa na mgombea huyo David Djumbe amewasilisha barua iliyosainiwa na Katibu wa CHADEMA wa Wilaya.
“Barua imesainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, wlaya ya Singida Vijijini Amani Mloya, tuhuma za kusema huyu sio mgombea wao si za kweli, huyu ataendelea kuwa mgombea mpaka atakapoamua kutumia haki yake ya kujitoa kama alivyotumia haki yake kugombea.” – Ramadhan Kailima

Post a Comment

 
Top