Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.

 afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa TFF na litatolewa majibu hivi karibuni.
"Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa", amesema Alfred Lucas.
Hapo jana Zitto Kabwe ametoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilinajaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biasha ra utumwa.Post a Comment

 
Top