Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Viongozi wa umma nchini wametakiwa kukabidhi orodha ya mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kabla ya Desemba 31 2017.
Agizo hilo limetolewa leo na Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.

“Utaratibu huo upo kwa mujibu wa sheria, hivyo lazima watekeleze kwa wakati, Viongozi wanafahamu wajibu wao, hivyo wafanye haraka iwezekanavyo wawasilishe hasa kwa kuzingatia muda uliobakia ni mchache”, amesema Jaji Nsekela.
Aidha Nsekela amewataja viongozi ambao wanatakiwa kuorodhesha mali zao ni wale wa kuteuliwa na kuchaguliwa na hiyo inawahusu pia viongozi wanaoelekea kustaafu.
Naye Ofisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti hiyo Bw. Filotheus Manula ameongeza kuwa ujazaji wa tamko la mali kwa viongozi wa umma ni takwa la kikatiba na kuna adhabu kwa wasiofuata ikiwemo kuonywa, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na wakati mwingine kufukuzwa kazi.

Post a Comment

 
Top