Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
RAPA anayekimbiza kwa sasa kutoka pande za Morogoro, Stamina amesema kwamba ngoma yao mpya walioimba na Roma Mkatoli (ROSTAM), wakimshirikisha Maua Sama, ‘Kiba_100’ haina matusi kama baadhi ya watu wanavyodai.

Stamina amesema hayo leo wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha XXL ya Clouds Fm kudai kuwa wanaosema ngoma hiyo ambayo ndani ya video yumo mtu mzima, Dk Louis Shika inastahili kufungiwa wanakosea.
“Ukisema hiki kitu kifungiwe, je kifungiwe kwa sababu gani? Kwenye wimbo huo hatujatukana hata kidogo, hakuna tusi ambalo lipo cleared ambalo mtu anaweza kusema hili ni tusi, hakuna tusi tulilotukana.
“Mimi na mwenzangu (Roma), katika uandishi tulifuata maadili ya kutofikisha vitu vingine kwa sababu ya ukali wa maneno. Ukisema wimbo ufungiwe ni sawa na kusema niache kazi yangu ya muziki. Then panakuwa hakuna uhuru wa msanii kwa sababu kuna vitu msanii atashindwa kuvifikisha. Kama umeongea kitu ambacho kina ukweli acha kifike,” amesema Stamina.

Post a Comment

 
Top