Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wolper Atoboa Siri ya Gharama ya Jino Lake la Silva 
HII ikufikie wewe mpenda ubuyu kuwa, lile jino la shaba ‘silva’ la staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe lililoleta gumzo mitandaoni, mwenyewe amelifungukia kuwa, limemgharimu kiasi cha dola elfu 3 za Kimarekani (zaidi ya Sh. Mil.6 za Kibongo).


Akichonga na Star Mix, Wolper aliwashangaa wanaosema na kuweka picha zikimuonesha akiwa na mapengo wakati alifanya hivyo kwa makusudi na kuweka la silva ili kuwa na muonekano tofauti wa meno yake.

“Watu wanaongea tu bila kujua. Pengo hili nimelipandia ndege kwa makusudi na kwa taarifa yao tu hili jino la silva nililoliweka limenigharimu dola elfu 3 (Mil.6),” alisema Wolper. 

Post a Comment

 
Top