Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wolper Atoboa Siri Kuhusu  Wazazi Wake 
Msanii wa filamu Tanzania ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wajasiriamali wanaopiga hatua, Jackline Wolper, ametoa siri jinsi alivyosuswa na wazazi wake kwa kuona anawadhalilsha, wakati amekuja Dar es salaam kuanza kujitafutia maisha.Jackline Wolper amesema kwamba kiuhalisia familia yake ni watu ambao wanajiweza, hivyo alivyoamua kufanya biashara ya umachinga katika soko la kariakoo familia yake haikufurahia, na kuamua kumtenga.

"Wolper alichuniwa nyumbani kwa sababu ya ile kazi ya kuuza sabuni, kwa sababu wazazi wangu walikuwa na wadhifa na walikuwa na uwezo wa kunimiliki mimi na kuweza kunipatia biashara nikaendelea na maisha yangu, lakini niliweza kuwadhalilisha na kwenda kariakoo kuuza sabuni kama machinga, promotion dawa za mswaki, nikawadhalilisha  kwa kufanya ile kazi, nikachuniwa na wazazi wangu karibuni mwaka au miaka miwili siongei nao", amesema Wolper

Wolper ameendelea kwa kusema kwamba kitendo hiko ni mifano tosha kwa vijana wanaotaka kuwa kama yeye, kwani alichokipitia kilimpa wakati huku mambo yakimuendea tofauti

"Hizo zote ni changamoto za maisha ambazo wadogo zangu wanatakiwa wazijue na wazipitie, lakini wasizipitie kwa ubaya, usimuudhi mzazi ili ufanikiwe, unaweza usifanikiwe, mimi niliwaudhi wazazi wangu nikawa sielewi mpaka nikaenda kuomba msamaha", amesema Wolper

Hivi karibuni msanii huyo amezindua app yake ambayo itakuwa na mambo na matukio mbali mbali kuhusu yeye, pamoja na kazi zake za sanaa na ujasiriamali.


 

Post a Comment

 
Top