Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Diamond, Tudd Thomas Washinda Tuzo Nigeria Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Muandaaji wa muziki, Tudd Thomas wote kutoka Tanzania wameshinda tuzo za African Entertainment Legends Awards (AELA) jana Desemba 3, 2017 jijini Lagos, nchini Nigeria.


Diamond Platnumz ameshinda tuzo ya kolabo bora ya mwaka 2017 kupitia wimbo wake wa FIRE aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria Tiwa Savage huku producer Tuddy Thomas akinyakua tuzo ya Muandaaji bora wa muziki kwa mwaka 2017 barani Afrika.

Wengine walioshinda tuzo hizo ni Davido kupitia wimbo wake wa Coolest Kid in Afrika kwenye kipengele cha ‘Best Music Video of the Year’, RunTown, Black Coffee na wengine wengi.

Tazama orodha kamili ya washindi wa Tuzo hizo za (African Entertainment Legends Awards 2017) .

Post a Comment

 
Top