Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amewaomba radhi mashabiki wake kufuatia kushindwa kufanyika kwa tamasha la Funga Mwaka na King Kiba.
Hapo awali muimbaji huyo alihaidi kufanya hivyo lakini kwa sababu zilizoko nje ya uwezo wake kitu hicho kimeshindikana kufanyika. Kupitia ukurasa wale wa Instagram Alikiba ameandika;

Hello fans, natumaini kila mmoja wenu amekuwa na wakati mzuri katika kipindi hiki cha sikukuu. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi kwa kushindwa kuwatimizia ahadi ya kufanya #FungaMwakaNaKingKiba kama ambavyo niliwatangazia mwanzo.
Haikuwa lengo langu ila kuna mambo yamejitokeza yaliyo nje ya uwezo wangu ambayo yamesababisha kutoweza kufanyika kwa tukio letu ambalo pia lingehusisha uzinduzi wa products zangu pamoja na wimbo wangu mpya.
Pia ameongeza kuwa hivi karibuni Mungu akijaalia atawapa taarifa mashabiki wake namna watakavyoufungua Mwaka. Alikiba kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Single’ aliyoshirikishwa na Abdu Kiba.

Post a Comment

 
Top